KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema vyombo vya habari zaidi ya 1200 vimesajiliwa na kuajiri makundi mbalimbali ya watu wakiwemo watangazaji na mafundi mitambo
Msigwa amesema hayo leo Desemba 18, alipokuwa kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) wakati wa mkutano wa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi na Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji.
Msigwa amesema serikali inaendelea kuboresha sekta hiyo ili kuleta mabadiliko chanya kwa kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria za habari
Advertisement
Amesema sekta ya habari imekuwa ikichangia mapato ya serikali kupitia kodi na matangazo na huduma mbalimbali
Kwa upande mwingine Msigwa amesema wanampango wakufunga kamera katika uwanja wa taifa ili kuwabaini wale wote wanaofanya uharibufu wa uwanja waweze kuchukuliwa hatua badala ya timu husika kupewa adhabu.