Na Ruja Masewa, JamhuriMedia, Mbeya
Mara baada ya kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amewararua akidai, kabla ya kuifundisha CCM reforms wafanye kwanza reform ndani ya Chama chao.
Msigwa alisema hayo leo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliohudhuriwa na Katibu mwenezi wa chama hicho CPA Amosi Makala.

Akizungumza huku akishangiliwa na wana CCM msigwa uwanjani hapo alisema, Mkakati wa Chama kile anaouita Mkakati BUTU, Mkakati dhaifu na Mkakati ulioshindikana kabla haujaanza.
Alisema nasema hivi kwa sababu, Neno la Mungu linasema; Nyumba ikifitimika haiwezi kusimama, hivyo wasiweke mpira kwapani bali warudishe mpira
kiwanjani ili wawe na uhalali wa kushindana.
Alidai Mwenyekiti wao alipokuwa akiomba kura alisema, anataka kufanya Reform kwenye chama chao, kilichokuwa kinatawaliwa na anayedai ni Nkurunzinza.
Aidha alisema, kama chama kile kinataka kuifundisha CCM kufanya reforms, wafanye kwanza kwenye chama chao, ndipo waifundishe CCM.

“Ili wawe na uhalali wa kuitaka CCM ifanye Reform, wafanye Reform kwanza kwenye chama chao, ndipo waifundishe CCM.
Kwa upande wake CPA Amosi Makala aliuliza wana CCM, Sungura na Mamba wakiwa majini, nani mzoefu? Wakaji Mambaaa!
“Mchungaji Msigwa ni Kada Makini wa CCM. Amekuwa Mbunge kwa chama kile Miaka 10, amekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Miaka Nane, Mjumbe wa Halmashauri Kuu miaka 10. Mimi Nimempa cheo cha Udaktari. Na kuanzia sasa kila Chadema watakapoweka mguu, mimi na Msigwa Mguu kwa Mguu tutakanyaga hapo.
Akiwachagiza CCM, Makala aliwabeza Chadema na kusema, “Niseme nisisemee!!… Semaa!! ….Walisema wanakuja kuzindua Kampeni hapa na kumpokea Msigwa. Lakini Msigwa huyo hapo!!!.

Hata hivyo Makala aliwashukuru na kupongeza wananchi kwa kuipa CCM Ushindi wa kura nyingi kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji na kujigamba kwamba walikuwa wanajaribisha mitambo!.

