Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amewataka wanachama wake kuhakikisha chama chao wanakwenda kujibu maswali ya kijamii katika maeneo wanayoishi, na si kila siku kujibu maswali ya kisiasa.

Mbowe ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, akifungua mkutano mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) ambapo amewataka wagombea wa BAWACHA kutogombea kwa sababu ya uchu wa madaraka au nafasi za kugombea ubunge.

“Tusiingie na kuijenga BAWACHA kwa sababu ya Ubunge na udiwani wa viti maalum, kila mmoja aingie kwa dhamira ya kuijenga jamii ya Tanzania ambayo inatambua uzito na umuhimu wa mwanamke katika jamii”

Aidha Mbowe ametoa agizo kwa wana- CHADEMA wote nchini kusaidiana inapotokea mmoja wao amepata matatizo ikiwemo msiba au tatizo lolote lingine.