Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa.

Mama Maria Nyerere akiwasili katika Viwanja vya Karimjee, kwa ajili ya shughuli ya kuaga mwili wa marehemu.

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hammad akisalimiana na Mama Maria Nyerere eneo la tukio.

Jeneza lenye mwili wa marehemu.

Kutoka kushoto ni Marais Wastaafu, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, Edward Lowassa na mkewe, mama Regina Lowassa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akiwasili msibani hapo.

Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Dkt Gharib Bilali akisalimiana na mzee Kikwete, katikati ni Waziri Suleiman Jaffo.

Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu akiwasili.

Samia akisalimiana na mzee Mkapa.

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa Waziri Mkuu wake kabla ya kujiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa wameungana na mamia ya waombolezaji na viongozi wengine wa nchi katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngiombale Mwiru leo jijini Dar es Salaam.

Mbali na Mama Samia, Lowassa na Kikwete, viongozi wengine wengine waliohudhuria ni Marais Wastaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Mama Maria Nyerere, maalim Seif Sharif Hammad, Mama Regina Lowassa, Waziri mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba, Spika Mstaafu na Pius Msekwa.

Wengine ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Suleiman Jaffo, DC wa kinondoni, Ali Happy, majaji na viongozi wengine wa dini na taasisi mbalimbali nchini.