Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Watumishi wa MSD wa kada ya udereva, wamejengewa uwezo kupitia mafunzo mbalimbali yanayoandaliwa na taasisi hasa katika eneo la huduma kwa wateja wakati wa usambazaji bidhaa za afya.
Mafunzo hayo yanayofanyika mkoani Morogoro yamekutanisha madereva wote wa MSD kutoka Makao Makuu na Kanda.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Kaimu Meneja wa Rasilimali watu Adolar Duwe, ameeleza kuwa mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa kwa Wataalamu wa usambazaji bidhaa za afya kwani yatawawezesha kuongeza uelewa juu ya huduma kwa wateja na namna ya kuhudumia wateja wa MSD.
Akizumgumza kwa niaba ya maderava wa MSD Bw. Erick Kaaya, amesema mafunzo hayo yamewaongezea ujuzi, kujiamini na uelewa wa masuala mbalimbali ya muhimu katika kuhudumia wateja. Aidha ameiomba Menejimenti ya MSD, kuratibu mafunzo hayo mara kwa mara, ili kuwajengea uwezo na kuongeza tija katika utekelezaji wa shughuli za taasisi.