Na mwandishi wetu, JAMHURI MEDIA, Dar es salaam
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila kwa huduma nzuri wanazotoa kwa jamii na kuwataka wataalamu kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na weledi kwa kuwa Watanzania wanategemea huduma wanazozitoa.
Dkt. Kikwete ametoa pongezi hizo leo alipotembela banda la Muhimbili Upanga & Mloganzila katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara maarufu SABASABA ambapo pia amepata fursa ya kupata huduma katika banda hilo.
“Hongereni sana kwa kazi nzuri na kubwa mnayoendelea kuifanya mkiwa kama Hospitali ya Taifa mnapaswa kuendelea kutoa huduma bora za afya nchini . Amesema Mh. Dkt. Kikwete
Banda la Muhimbili linapatikana katika Ukumbi wa Kilimanjaro ambapo huduma mbalimbali zinatolewa ikiwemo huduma za Magonjwa ya Dharura, Lishe, Macho, ushauri kuhusu afya ya usikivu, vipimo vya msingi vya maabara pamoja na vipimo ya Ultrasound na ECG.