Na Happy Lazaro,JamhuriMedia, Arusha
SERIKALI imesema mradi wa Tanzania ya Kidijitali unaofadhiliwa na. Benki ya Dunia umefikia asilimia 80 ya utekelezaji 1wake, lengo likiwa ni kuweka mazingira wezeshi, kutoa huduma bora na miundombinu wezeshi kwa wananchi ili wanufaike na mradi huo.
Aidha mradi huo ambao unasimamiwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma umefanikisha kupeleka wataalamu 50 kusoma shahada ya pili na wengine 400 kupata mafunzo.

Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Mifumo na Huduma za Tehama kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia Mohammed Mashaka wakati wa kufunga kikao cha kufanya tathimini ya hafua zilizofikiwa za kufanya mradi huo, amesema mradi huo ambao ulianza mwaka 2021 utakamilika Oktoba 2026.
Amesema lengo la mradi huo kuwezesha wananchi kupata huduma wakati wowote na mahali popote ili kufikia malengo ya uchumi wa kidijitali.
“Mradi huu mpaka sasa umefanikisha kuunganisha mifumo ya Taasisi 901 kusomana, minara 758 imeondolewa kutoka 2G kwenda 3G pamoja na kuhuishaa vifaa ambavyo vimeshasimikwa,kuongeza uwezo wa Intaneti katika Taasisi za serijali ambapo Tanzania Bara inatumia GB 40 na Zanziba GB 20.”amesema.
“Pia mradi huu umefanikisha kutengeneza vituo 30 vya kuwezesha wananchi kupata huduma muhimu sehemu moja, pamoja na kutengeneza mifumo ya kutoa huduma ambayo jamii namba, jamii ‘X-change’ na mfumo wa huduma za malipo (Cashless).amesema .

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mkataba,Kazi Serikalini Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Priscus Tairo amesema mradi huo umesaidia serikali kutumia mfumo wa kielekroniki wa upimaji utendaji kazi kwa watumishi wa umma (PERMIS &PIPMIS na tathimini ya mahitaji ya rasilimali watu.
Kiongozi wa Timu ya wataalamu wa mradi huo kutoka Benki ya Dunia (WB) Paul Seaden alisema, mradi huo unaendeshwa kipindi cha miaka mitano ambapo unashughulikia maeneo Anuwai, zinazounga mkono nguzo tofauti za mkakati wa uchumi wa dijiti, ikiwemo kuwainua wananchi kiuchumi maeneo ya vijijini.
Amesema lengo kuu ni kuwafikia watanzania kupata huduma za uhakika katika kiwango kinachotakiwa cha utoaji wa huduma za dijiti kwa serikali, ikiwemo uanzishwaji wa vituo vya duka moja nchini kote pamoja na kuanzisha mtandao wa vituo vya utoaji wa ujuzi wa dijiti na uandishi wa dijiti .

” Tumekuwa tukiendesha mradi huu kwa miaka mitatu sasa, na kwa hivyo dhamira hii ni hatua muhimu katika maisha ya mradi huo, kwani tunaangalia miaka miwili iliyopita na tunaanza kuunda sehemu za mwisho za utoaji zinaonekana kwa mradi huo,”amesema.
Ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika uchumi wa kidigiti, ambayo yamefanywa hadi sasa na kufikia asilimia 80, ya utoaji huduma kimifumo pamoja na jamii kwa ujumla, lakini pia mradi huo umehusisha makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu.