Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dodoma

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeshiriki maonesho ya kitaifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) kwa kutoa elimu kwa magonjwa ya mifupa pamoja na masuala ya lishe.

Akizungumza na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika maonesho hayo ambayo yanaendelea jijini Dodoma, Daktari wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu, Consolata Shayo kutoka Taasisi ya Tiba amesema taasisi hiyo pia inatoa huduma za kibingwa katika maonesho hayo.

“Pia katika maonesho haya wagonjwa wengine tuliowapokea ni wale wenye matatizo ya mifupa, mgongo, kichwa, mishipa ya fahamu ambapo huduma hizo zinatolewa bure katika banda la MOI.

“Vilevile tunatoa elimu kwa masuala ya lishe kwa wale ambao wana uzito mkubwa na wenye lishe duni yaani ambao wana uzito mdogo kuliko urefu,” amefafanua.

Dkt. Shayo amewashauri wananchi ambao bado hawajafika kwenye banda la MOI kuhakikisha wanafika ili waweze kusaidiwa kupatiwa huduma za kibingwa.

“kwa wale ambao wanahitaji matibabu zaidi tunawaandikia Rufaa ili waweze kwenda Hospitali kubwa na wengine tumekuwa tukiwaandikia dawa. Mfano kazi zetu tunazozifanya tunakaa muda mrefu bila kifanya mazoezi kukaa zaidi ya dakika 45 hadi lisaa bila kunyoosha miguu na mgongo kuna changia kuumwa mgongo pamoja na miguu, “amesema.

Amesema kuwa kutokana na aina ya maisha ambayo jamii imekuwa ikiishi hapo awali na ambavyo wanaendelea kuyaishi kwa sasa yanachangia kuleta madhara ya lishe.

Please follow and like us:
Pin Share