Na Dotto Kwilasa,JamhuriMedia,Dodoma

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu (MOI) Balozi, Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema Taasisi hiyo imefanikiwa kuanzisha huduma zaidi ya 10 za kibobezi ambazo hapo awali ziliwalazimu wagonjwa kuzifuata nje ya nchi.

Amezitaja huduma hizo kuwa ni upasuaji na uchunguzi wa ubongo bila kufungua fuvu ambapo hadi sasa wagonjwa 62 wamehudumiwa,upasuaji wa Nyonga na magoti wa marudio wagonjwa 74 qamehudumiwa na Ulupasuaji wa mgongo kwa njia ya matundu ambapo wagonjwa 17 wamefanyiwa.

Mkurugenzi huyo ameeleza hayo leo March 5,2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ameeleza kuwa wagonjwa 41 wamepata Matibabu ya kiharusi kwa kupitia mishipa mikubwa ya damu ya paja .

“Huduma nyongine upasuaji wa kunyoosha mgongo uliopinda (Kibion0go) wagonjwa 64 wamehudumiwa.
Kuondoa uvimbe kwenye ubongo kupitia tundu la pua , wagonjwa 41 wamehudumiwa,huduma ya maumivu sugu ya mgongo, wagonjwa 607 wamehudumiwa na huduma ya wagonjwa maalum na wagonjwa wa kimataifa, wagonjwa 6,106 wamehudumiwa, “amesema

Balozi Ulisubisya amesema huduma ya mkono wa umeme mpaka sasa wagonjwa 6 wamewekewa mkono bandia na kutengeneza viungo bandia kwa teknolojia ya ‘3D’ kwa wagonjwa wanne (4).

Amesema Taasisi ya MOI imeendelea kutoa huduma nyingine za kibingwa Bobezi na kupunguza rufaa za kupeleka wagonjwa nje ya nchi ambapo upandikizaji wa nyonga bandia wagonjwa 728 wamehudumiwa,
Upandikizaji wa goti bandia wagonjwa 636 wamehudumiwa,Upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu wagonjwa 1,115 wamehudumiwa na upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo (Aneurysm) 14 wamehudumiwa.

Huduma nyingine ni Upasuaji wa mfupa wa kiuno wagonjwa 395 wamehudumiwa Upasuaji wa kichwa kikubwa na mgongo wazi watoto 1,797 wamehudumiwa,Upasuaji wa ubongo kwa kufungua fuvu 815 na upasuaji wa mgongo wagonjwa 1,061 wamehudumiwa.

Ameeleza kuwa katika kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2021, Taasisi ya Mifupa MOI imehudumia jumla ya wagonjwa 816,383 kama wagonjwa wa nje na wale wa dharura (OPD na EMD), ambapo kumekuwa na wastani wa ongezeko la wagonjwa 3,023 kwa mwaka.

Kwa upande wa wagonjwa wa ndani (IPD), jumla ya 35,170 walihudumiwa, ikiwa ni wastani wa ongezeko la wagonjwa 453 kila mwaka. Aidha, wagonjwa 30,289 walifanyiwa upasuaji, ambao ni sawa na 86.2% ya wagonjwa waliolazwa na Kwa sasa MOI ina jumla ya vitanda 362, Madaktari 129 na Wauguzi 518 .

Amesema Taasisi ya MOI imefanikiwa kutoa huduma za kibobezi kwa wagonjwa 7,366 ambapo gharama za matibabu haya ndani ya nchi zilikuwa Shilingi za Kitanzania bilioni 68,451,603,600.00 na kama wagonjwa hawa wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu jumla ya shilingi bilioni 218,280,169,470 zingetumika.

“Hivyo serikali imefanikiwa kuokoa shilingi bilioni 149,828,565,870.00 ambazo zimetumika katika shughuli nyingine za maendeleo ikiwemo kununua mashine za kisasa za kupumulia (ICU Ventilators), Monitors, Vitanda na Ambulance ya kisasa (Vyenye thamani ya Tsh billion 1.3), “amesema.

Amefafanua kuwa Serikali imetoa Tsh Bilioni 4.4 kwajili ya ununuzi wa mashine mpya ya kisasa ya MRI na CT scan kwa lengo la kuhakikisha wagonjwa wanapata huduma hiyo kwa uhakika na wakati bila ya kusubiria huduma muda mrefu.

Kuhusu maslahi ya watumishi katika kipindi cha miaka minne amesema Taasisi ya MOI imefanikiwa kupandisha vyeo watumishi 842 na kuajiri watumishi 210.

Amesema Taasisi imeendelea kuwa na ushirikiano mzuri na Taasisi mbalimbali za kimataifa katika kufanya kambi za upasuaji, mafunzo kwa wataalamu wetu, Tafiti na misaada ya vifaa Tiba na taasisi iliingia mkataba wa ushirikiano na Chama cha madaktari cha nchini China (CMA) na Hospitali ya Tian Tan ya Beijing Peking China Katika kuendeleza fani ya upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya fahamu.

“Tumeendeleza ushirikiano na hospitali ya Ramaiah ya Bengaluru India Katika kuendeleza fani ya Upasuaji wa kurekebisha mishipa ya damu kichwani pasipo kufungua fuvu la kichwa ikiwa ni pamona na kuwa na ushirikiano na hospitali na taasisi nyingi za ndani na nje ya nchi ambazo zinaendelea kujengea uwezo wataalamu wetu na zingine tunazijengea uwezo sisi,”amesema.