Na Cresensia Kapinga, Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,Kanali Laban Thomas amewaasa wakazi wa Vijiji vilivyo jirani na daraja la mto Mhuwesi wilayani Tunduru kuona umuhimu wa kutunza mazingira pamoja na miundo mbinu ya Daraja hilo ili liweze kupitika kwa wakati wote hasa ikizingatiwa kuwa liko kwenye barabara kuu ya kutoka Songea kwenda Mikoa ya Kusini Lindi na Mtwara, Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam na Nchi jirani ya Msumbiji.
Ameyasema hayo jana wakati akipokea taarifa ya urejeshaji wa Daraja la mto Mhuwesi ambalo awali lilikuwa limesogezwa na maji katika kipindi cha msimu wa mvua zilizokuwa zinanyesha kipindi hicho na kusababisha mafuriko na barabara ililazimika kufungwa ili kupisha matengenezo ya kuliudisha daraja la zege mahali pake.
Alisema kuwa serikali ilishalidhia kutoa fedha Zaidi y ash. Biloni 1.55 kwaajiri ya kuresha sehemu yake daraja hilo baada ya mvua kulisogeza na kwenda sehemu nyingine hivyo ni jambo la serikali kupongeza kwa kazi nzuri ya kusikiliza kero mbalimbali ambazo zilikuwa ni kikwazo kwa wananchi wakiwemo wafanya biashara ,wasafirishaji pamoja na abilia.
Kanali Thomasi alisema kuwa viongozi wa serikali wilaani humo wanapaswa kuzingatia sheria za mazingira ikiwemo wakulima kufuata taratibu zilizopo za kibinadamu kufanya shughuli mita sitini kutoka kwenye kingo za mto na amewaonya watu wenye tabia ya kupita kuchimba madini kando kando ya mto hivyo ameuagiza uongozi Wilaya hiyo kuchukuwa hatua haraka pindi wanapowabaini kwani kufanya hivyo ni kuharibu maingira ya Mto ambao mvua zikinyesaha husababisha mafurikoa na kuharibu miundombinu ya madaraja.
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amewapongeza wataalam ( Wahandisi ) wa wakala wa barabara (Tanrods) nchini pamoja na mkandarasi wa Kampuni ya Mtwivila ya kutoka mkoani Iringa ambao walifanya kazi nzuri na kuweza kufanikisha kulisukuma daraja hilo la zege lenye uzito wa tani 2000 ambalo linauwezo wa kupitisha magari yenye uzito Zaidi ya Tani 100.
Kwa upande wake Meneja wa wakala wa barabara (Tanirods) Mkoa wa Ruvuma Mhandis Mlima Ngaile amesema kuwa daraja la mto muhuwesi awali lilijengwa kupitia mradi wa barabara ya Tunduru Mangaka na Matambaswala yenye urefu wa Km. 202 kwa kiwango cha lami chini ya ufadhili wa AFDB .
Alisema kuwa mnamo Februari 14 mwaka jana kulitokea mafuriko na atimaye kujaa kwa mto Mhuwesi na kufurika daraja la mto huo katika barabara ya Songea Tunduru Mtwara ambapo daaja hilo lilifunikwa kabisa na maji ya mto huo na kusambaa umbali wa takribani mita 100 wa pande zote za maingiio za daraja hilo na baada ya kutokea tukio hilo ofisi ya Tanrod Ruvuma kwa kushirikiana na uongozi wa Wilaya ya Tunduru ililazimika kufunga barabara na kuzuia matumizi ya sehemu hiyo kwa kipindi chote cha mafuriko.
Mhandizi Ngaile alisema kuwa baada ya kujilidhisha kuhusu uimara wa daraja magari yalianza kuruhusiwa upande mmoja wa barabara ili kuepusha madhara mengine amabyo yangeweza kujitokeza kama daraja hilo kama lingeruhusiwa kutumika pande zote.
Alisema kuwa kuleta timu ya wataalam wa madaraja kutoka makao makuu kuja kufanya shughuli za uchunguzi wa kina chini ya kitanda cha daraja kwa kutumia gari maalum la ukaguzi na kuweka alama za kutosha na kuongoza magari na kuongoza usalama wa watumiaji jambo ambalo lilifanywa chini ya usimamizi wa Tanroad Ruvuma na kwamba kwa sasa wameshafanikiwa kulilejesha daraja hilo mahali pake ambapo wataalam ambao ni wahandisi kwa pamoja kutoka mikoa yote Tanzania walifanya kazi nzuri na walifanikiwa kulisukuma daraja na kulirejesha mahali pake kwa kushilikiana na mkandarasi mzawa.
Kwa upandewao baadhi ya wananchi wa vijiji vilivyopo jirani na daraja hilo wameipongeza serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa jitihada za kulirejesha daraja hilo na kuanza kutumika na kwamba wamesema serikali ni vyema wakaendelea kuwaamini wakandarasi wazawa wa ndani badala ya kuwapa kipaumbele wakandarasi kutoka nje ya Nchi.