Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan amewavisha nishani mbalimbali, Maafisa na Askari wa JWTZ Kanda ya Songea.
Miongoni mwa waliovishwa nishani ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abass Ahmed ambaye ametunukiwa Nishani ya Utumishi Uliotukuka,Nishani ya Utumishi Mrefu,Nishani ya Miaka 60 ya Muungano na Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ.
Akizungumza baada ya kuwavisha nishani, Jenerali Mkunda amewapongeza Maafisa na Askari waliotunukiwa nishani hizo kwa na kumshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan alivyotambua mchango wao katika kulitumikia taifa kwenye nyanja ya ulinzi.
Jenerali Mkunda amewataka Maafisa na Askari kuendelea kuviishi viapo vyao na kuhakikisha mipaka yote ya nchi yetu inakua shwari na salama wakati wote.
Nishani walizotunukiwa ni pamoja na Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Utumishi Mrefu, Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema, Nishani ya Miaka 60 ya Muungano,Nishani ya Miaka 60 ya JWTZ pamoja na Nishani ya Ulinzi wa Amani ya Jumuiya ya SADC.
