Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amewasili nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri wilayani Butiama Mkoani Mara tarehe 03 Novemba 2024 kwa ajili ya kutoa salamu za pole kwa wafiwa na kukagua maandalizi ya Mazishi ya Hayati Jenerali Musuguri yatakayofanyika tarehe 04 Novemba 2024.

Jenerali Mkunda amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kuwashukuru wananchi wa Butiama na maeneo ya karibu kwa kushiriki katika kutoa heshima za mwisho kwa marehemu ikiwa ni heshima kwa kiongozi huyo aliyetoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa taifa letu.

Jenerali Musuguri aliyefariki tarehe 29 Oktoba 2024 akiwa na umri wa Miaka 104 atazikwa nyumbani kwake kwa heshima zote za kijeshi.