Katika ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere mazingira ya nje ya ukumbi yana mvuto wa kipekee kutokana na kuwepo kwa burudani za aina mbalimbali.
Mkutano huu wa Nishati unaunganisha wageni na viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi hususa ni katika bara la Afrika.
Kila kona ya ukumbi shughuli za utamaduni zinaendelea huku wageni wakishuhudia ngoma za makabila mbalimbali kutoka sehemu tofauti za nchi.
Ngoma hizi za makabila mbalimbali zinatoa ujumbe unaohamasisha matumizi ya Nishati Safi.
Wageni wanaofika katika ukumbi huu wanapata fursa ya kujivunia na kuelewa zaidi utamaduni wa nchi hii.
Huku mijadala inayoendelea ikiwa ni kuhusu teknolojia ya nishati, matumizi bora ya nishati na mikakati mbalimbali ya maendeleo kuhusu Nishati.
Mkutano huu unawaunganisha wadau wa sekta ya nishati kwa namna ya kipekee na ni fursa nzuri kwa wadau wa ndani na nje ya nchi kubadilishana mawazo na kujifunza kutoka kwa wataalamu wa sekta hiyo. Hii ni sehemu muhimu ya kujenga mustakabali bora wa nishati ya Tanzania na dunia kwa ujumla.