Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mara

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Usambazaji Umeme Tanzania (TANESCO) Gissima Nyamo-Hanga amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Aprili 13,2025 kwa ajali iliyotokea Wilayani Bunda Mkoani Mara

Mkuu wa Mkoa wa Mara Evansi Mtambi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo amefafanua kuwa tukio limetokea kati ya saa 6hadi 7 usiku wa kuamkia leo.

” Ni kweli tukio lipo na Gissima amefariki Dunia na RPC atakuwa na taarifa kwa kina amesema ” Mtambi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidia kutoa taarifa kwa kina badae kidogo

Naye Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara Nicksoni Babu amebainisha kuwa Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali Teule Wilaya ya Bunda huku wakisubiria taarifa zaidi na taratibu nyingine

Aidha Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake libarikiwe Jamhuri inatoa pole kwa Menejimeti ya Tanesco ndugu jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mpendwa wao.