Aliyewahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu mwanzilishi na baadaye Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom PLC, Michael Joseph amejiuzulu wadhifa wake, taarifa ya Safaricom imesema uamuzi huo umefanyika Agosti 1.

Joseph, ameshiriki kuongoza kampuni hiyo katika nafasi mbalimbali tangu 2000, ikiwa ni pamoja na kuwa Afisa Mtendaji Mkuu mwanzilishi. Pia amehudumu katika nyadhifa mbalimbali kama meneja mkuu, mara mbili kama afisa mkuu mtendaji na mara moja kama mwenyekiti wa bodi.

Wakati wake Safaricom, Joseph alichangia pakubwa ukuaji wa kampuni, akiichukua ikiwa na wateja 18,000 mwaka 2000 hadi kufikisha wateja zaidi ya milioni 17 wakati wa kustaafu kwake Novemba 2010.

Mabadiliko hayo yaliifanya Safaricom kuwa kampuni ya mawasiliano iliyofanikiwa zaidi  Afrika Mashariki.