PSRC waagizwa wamlipa Msira
Katika kipindi ambacho mgogoro huo ulikuwa unaendelea miaka ya 2000, aliyekuwa msaidizi wa Waziri wa Mipango wakati huo, Dk. Juma Ngasongwa, aliandika barua PSRC kushinikiza imlipe Msira fedha hizo alizoingia mkataba na Jiji la Dar es Salaam, kuwa magari ya METL yakikatiza kwenye kiwanja chake yalipa Sh 500,000 kila siku.

Fedha hizo hazikupata kulipwa kwani baada ya PSRC kuvunjwa, shughuli zake zikahamishiwa kwa Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC), wao waligoma kumlipa na deni hilo ndilo linaloonekana kwenye vitabu vya CAG kuwa DRTC inaidai Serikali Sh bilioni 2.34.

METL wajaribu kununua kiwanja Na 10
Mwaka 1999 METL walipeleka ofa ya kununua kiwanja hiki Na 10 kwa PSRC na wakaahidi kuwa wangeweza kulipa dola 300,000 lakini PSRC ilikataa kuwauzia kiwanja hiki kwa maelezo kuwa fedha walizoahidi kutoa ni kidogo, hivyo waongeze bei hadi dola 500,000.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa baada ya pendekezo hilo pande zote mbili zilikaa kimya hadi mtaalamu Mkulo alipokutana na uongozi wa METL Juni 8, 2010.