Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ,amesema mwamko wa kufanya mageuzi ya elimu ni ajenda iliyopo duniani na kwamba Tanzania imewahi kuanza mageuzi hayo.

Hayo ameyasema leo Desemba 6,2022 jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa mwaka wa kufanya mapitio ya sekta ya elimu ambapo amewaomba wadau hao kushiriki katika mageuzi hayo.

Prof.Mkenda amewapongeza wadau kwa namna wanavyoshiriki kikamilifu kutoa maoni yao madhubuti kwa ajili ya kusaidia mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini.

”Sekata ya elimu nchini bado inahitaji mageuzi makubwa hivyo anaamini kupitia mkutano huo Wadau watapata nafasi ya kujadi kikamilifu namna ya kuleta maendeleo endelevu kwenye sekta ya elimu.

“Baada ya Rais Samia kuingia madarakani alitoa maelekezo ya kufanya mapitio ya Sera na mabadiliko ya mitaala kwa lengo la kuhakikisha elimu inayotolewa inaendelea kuwa bora na kutoa elimu ujuzi. Niwaombe wadau tuendelee kushirikiana katika kuboresha na kukuza elimu nchini,” amesema Prof Mkenda.

Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu Tanzania  Bi.Faith Shayo,akitoa maoni wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

Aidha Waziri Mkenda aliwataka wadau hao kuwa mapitio ya sera na mitaala yameshirikisha wadau mbalimbali na kwamba kwa sasa yapo tayari kwa mjadala wa kitaifa kuhusu mapendekezo ya sera ya elimu na mitaala.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Francis Michael amesema kila mmoja aliyepata fusa ya kushiriki mkutano huu kujadili kwa kina mada zitakazowasilishwa na kutoa maoni yenye tija katika kuimarisha na kuendeleza elimu yetu nchini.

” Wizara inaendelea na maboresho ya mitaala kuanzia ngazi ya Elimumsingi hadi Elimu ya juu,uboreshaji wa Sera ya Elimu unaendelea baada ya ukusanyaji wa maoni ya wadau wa elimu nchini kote na kuendelea kuyachakata,” alisema Dkt.Michael.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bw.Ocholo Wayoga,akizungumza  wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

Pia Dkt.Michael alisema Kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imeandaa miongozo ya utoaji wa elimu kwa kutumia TEHAMA kwa elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu na Kukamilisha Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu 2021/22 -2025/26.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu Tanzania Bi.Faith Shayo amesema kuwa mkutano huo umekuja Muda Muafaka kwani Dunia kupitia Umoja wa Mataifa ipo katika mabadiliko na mageuzi katika Sekta ya elimu kuanzia Sera,Miongozo na Mitaala yake ili kuleta mageuzi yenye tija.

Sehemu ya Wadau wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu pamoja na wanafunzi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa  Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Desemba   6 mpaka 7 Jijini Dodoma.