Dar es Salaam
Na Mwl Paulo S. Mapunda
Novemba 2019 viligundulika virusi vinavyosababisha ugonjwa wa corona nchini China. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), tangu wakati huo hadi sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni tano wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
Takriban miezi 24 baadaye (2+4=6), yaani Novemba, 2021, WHO ikatangaza aina mpya ya kirusi (fourth variant) na kukipachika jina la ‘OMICRON’, neno lililotoholewa kutoka lugha ya Kigiriki.
Hiki ni kirusi cha nne cha corona kugundulika tangu Novemba 2019, ni kama tunashuhudia mfululizo wa virusi!
Hiki ni miongoni mwa virusi vya mwisho mwisho kuelekea mfumo mpya wa ulimwengu (kwa Kiingereza New World Order).
WHO imetangaza kuwa kirusi OMICRON ni cha kutia hofu kutokana na tabia zake za kubadilikabadilika na kusambaa kwa kasi.
Halikadhalika tafiti za kisayansi zinaonyesha kwamba OMICRON kinashambulia zaidi vijana tofauti na kile cha awali ambacho kinashambulia zaidi wazee!
Katika wimbi hili la nne la corona, nawaasa Watanzania wenzangu kuwa macho zaidi na kuchukua hatua zote muhimu kujikinga na janga hili kwa kuwa ugonjwa huu si kudra za Mwenyezi Mungu, bali ni kazi ya shetani akishirikiana na mawakala wake ambao wamekubaliana na matakwa ya kishetani.
Yeyote anayehisi kuwa kuna mkono wa Mungu katika ugonjwa huu basi anakosea sana. Mungu hakumuumba mtu ili afe, hapana! Kifo ni matokeo ya dhambi iliyochukua mimba na kuzaa mauti.
Nawaasa Watanzania wenzangu kwa kuwa siku ya Alhamisi (yaani siku ya sita) kwa mujibu wa kalenda ya Kiarabu, Desemba 9 (12=2×6), mwaka 2021, taifa letu lilitimiza miaka 60 (yaani 6+0=6) tangu tupate uhuru wetu kutoka kwa Waingereza, taifa linalosemwa kuwa na idadi ya watu zaidi au sawa na milioni 60 (yaani 6+0=6), unaweza kuona jinsi namba sita (6) zinavyoongozana katika tukio zima lihusulo uhai wa taifa hili.
Hata tarehe ya uhuru (9) ukiigeuza chini – juu kwa msingi wa ‘let them understand vice versa’ inakuletea namba sita!
Kwa kuzingatia kanuni ya namba na hesabu, Tanzania iko katika mstari wa hatari zaidi ukilinganisha na majirani zetu.
Tuko hatarini si kwa sababu ya namba sita kujirudia rudia, bali sababu ya kiroho ni kwamba nchi hii ni lango (spiritual portal) kwa sababu ya uwepo wa mlima mrefu kuliko yote barani Afrika; Mlima Kilimanjaro.
Hili linasukumwa hali kadhalika na uwepo wa ziwa lenye kina kirefu zaidi katika Bara hili la Afrika; Ziwa Tanganyika.
Hali hiyo inasababisha kila jambo linalopangwa kuhusu Afrika liiguse Tanzania moja kwa moja. Nafasi na nguvu iliyonayo Tanzania kiroho, inasababisha tusiwe salama hususan mipango miovu inapopangwa kuhusu Bara hili la Afrika.
Mpango mkuu wa kimasonic ni ule wa kupunguza idadi ya watu duniani na kubaki bilioni moja tofauti na mpango wa Mungu wa mbinguni wa; “enendeni duniani kote mkazaane na kuongezeka mkaijaze nchi.” (Mwz. 1:28).
Ili kufanikisha lengo lao hilo, wanaotumia mbinu za mumiani na za kihayawani, mathalani matumizi ya kondomu na njia nyingine ovu za uzazi wa mpango, huharibuji mimba, ongezeko la kuvunjika kwa ndoa, ushoga na ndoa za jinsia moja, kuongezeka kwa ufuska na umalaya duniani.
Pia vita ya wenyewe kwa wenyewe na vita baina ya mataifa, ugaidi duniani kote, majanga ya asili na majanga ya kutengenezwa, ukame na ongezeko la joto duniani, ongezeko la magonjwa ya kuambukiza, ongezeko la mmomonyoko wa maadili kupitia simu janja na vyanzo vingine vyenye programu laini.
Utu wa mtu (dignity of a human person/being) unazidi kupotea, ile nguvu ya asili ya kiumbaji itokanayo na agizo la Mungu muumbaji kwa msingi wa kanuni ya dhahabu (golden rule) ipatikanayo katika Mathayo 7:12 imeyeyuka kama barafu juani.
Binadamu wanafanana kwa hali zote na hayawani wa mwituni, amri kuu ya upendo inapigwa kumbo mchana kweupe, haki imekuwa msamiati mgumu usioweza kutekelezeka si kwa watawala pekee bali hata kwa watu wa kawaida.
Wenye nacho wanaendelea kujilimbikizia zaidi, wasionacho hata kile kidogo wananyang’anywa, maskini na fukara wanaendelea kufukarishwa zaidi na mifumo nyongefu inayaotawala dunia.
Watoto wa maskini wanakosa lishe bora, elimu bora, matibabu bora, makazi bora na maji safi na salama ya kunywa.
Pamoja na binadamu kujaribu kujitutumua ili kujiweka huru tangu nguvu zisizoonekana zinazozinga maisha yake, lakini bado ameendelea kuwa muathirika wa kisichojulikana, nguvu ya kuwapo na kutokuwapo.
Tuko leo kwa kuwa Mungu amependa tuwepo lakini nguvu kinzazi dhidi ya uwepo wa mtu inatamani kutuangamiza wote.
Neema ya Mungu inaendelea kututetea sisi sote na kutuhakikishia uhai na tumaini la maisha baada ya kifo (perpetuity), kwa kuwa aliyemuumba shetani ndiye aliyetuumba sisi.
Kwa sababu hiyo hatupaswi kumuogopa shetani bali yule aliyemuumba ambaye ni Mungu (The Lord of hosts).
Tuwasiliane: [email protected]; 0755 671 071.