Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Wakati Serikali inapanga mikakati ya kuwasadia vijana katika kilimo, imeonekana changamoto kubwa ya vijana kuingia kwenye kilimo ni mitaji.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Hotel ya Serena Jiji baada ya kufungua mkutano wa kongamano la wadau wa kilimo.
Bashe amesema changamoto ya mitaji kwa vijana ipo kwa muda mrefu, ndiyo maana wamekaa na wadau wa Maendeleo waone namna ya kupeleka pesa hizo moja kwa moja kuwanufaisha wakulima badala ya kongamano na warsha.
Amesema kwa sasa tatizo la mifumo ya benki, bado haijawa rafiki kwa kijana anayetoka Chuo Kikuu kuingia moja kwa moja kwenye kukopa kwa ajili ya kilimo ,ana weza kuwa na wazo zuri la shughuli za kilimo akitengeneza andiko cha kwanza ataulizwa dhamana kitu ambacho hana.
“Kama tunavyojua baada ya mtu kukopa kwa ajili ya wazo la biashara, kinacholipa mkopo sio zamana ni shughuli ya kiuchumi kwa hiyo tunajaribu kusukuma hizi ajenda ni lazima zibadilike.
Mwaka huu mwezi wa pili serikali imekuwa na majadiliano makubwa na Wizara ya
Kilimo, Mifugo na uvuvi ,lengo lilikua kuwepo kwa kitu kinachoitwa Agriculture Finance Policy kwasababu hakuna mtu anawekeza kwenye kilimo miaka miwili mitatu akalipa mkopo si kweli kwa hiyo lazima tuwe na stong agriculture finance policy .
Mheshimiwa Rais kafanya jitihada kubwa, kulazimisha Mabenki ya biashara kushusha liba kwenye mikopo sambamba na kuwafanya vijana kubadilisha mitazamo yao na kujikita katika shughuli za kilimo.
Kwa sasa ndani ya Serikali tunajadiliana kuwa na Agriculture finance policy ,ili Mfugaji aweze kukopeshwa, Mvuvi na Mkulima waweze kupata mitaji ambayo ni ya muda mrefu kwasababu kilimo ni Uwekezaji wa muda mrefu hivyo lazima tuwe na strong policies ambazo zitatupeleka huko.
Kwa muda mrefu tumekuwa wenzetu wadau wa maendeleo, wakitupatia fedha za kwenda kwenye sekta ya kilimo nyingi zilikuwa zina kwenda kwenye warsha na makongamano.
Kwa hiyo mjadala mkubwa tunataka wenzetu wadau wa maendeleo,fedha wanazoleta zihame kwenye kutupatia mafunzo na kwenye kutatua matatizo ya msingi ya Mkulima.
Ameongeza kuwa kwasasa wadau wa naendeleo, wanatarajia kusaini makubaliano ambayo yata onyesha maeneo ya msingi ya kuwekeza fedha pamoja na Serikali.
Bashe amesema kwa sasa ,hata fedha za Serikali za maendeleo zimekuwa zinapelekwa kwenye maeneo ya utafiti ,uzalishaji wa mbegu,mbolea ambapo mitazamo inawahusu wao hata sisi kubadilika.
Akizungumza kuhusu jitihada za kuinua uchumi wa blue,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Edwin Mhede,amesema baada ya Serikali kutambua eneo hilo linaweza kutoa mchango mkubwa, imewekeza kiasi cha bilioni 289 kwa ajili ya kujenga bandari kule Kilwa Masoko na matarajio kufikia mwezi February 2025 itakuwa imekamilika.
Mhede amesema ujenzi wa bandari una husiana na miundombinu ya kuwezesha sekta ya uzalishaji, kwenye muktadha wa maendeleo
Tunaangalia sana nguzo tatu lengo ni kuhamasisha Wavuvi watoke kwenye maji madogo, waende pia kwenye maji makubwa kwani huko ndiyo watapata samaki wengi na wazuri ambao wanaweza kuchagiza maendeleo makubwa kwenye eneo hili
Amesema sambamba hilo kutakuwa na Mwambao kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vya kuchakata Samaki, hapo sasa kutakuwa na mnyororo wa thamani kama sehemu ya kunufaika na uchumi wa blue.
Serikali imewekeza fedha za ndani bilioni 289 kuchagiza maendeleo ya uchumi wa blue lakini pia uko chini ya mamlaka inayosimamia uchumi huo na inafanya kazi pande zote mbili Tanzania na Zanzibar.
Yenyewe imejiimaisha kuzithibiti na kuchochea maendeleo ya kuhakikisha wavuvi kutoka ndani na nje ya nchi, wanapata vibali kwa pamoja ili kuhakikisha wanakwenda kwenye maji makubwa.