Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Wilaya ya Temeke umekimbizwa umbali wa KM 81.78 Kukagua, kuweka jiwe la msingi, pamoja na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mwenge wa Uhuru 2024 umeendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia Ujumbe maalum unaosema “Uhifadhi wa Mazingira na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pia Ujumbe wa kudumu wa Mbio za Mwenge katika mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya na Rushwa.
Vilevile Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Temeke umekagua, umezindua na kuweka jiwe la msingi miradi mbalimbali kama Mradi wa Polyclinic wa vijana kupitia mikopo ya 10% (4% ya vijana), Watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Jeshi la wokovu Miburani, Barabara ya Mivinjeni Bandari Km 2.1 kiwango cha Zege, Ujenzi wa Bweni, bwalo,jiko, sehemu ya kunawia mikono na upandaji miti katika shule ya Sekondari Kibasila, Ujenzi wa jengo la upasuaji zahanati ya mbande, Mradi wa Kibao Complex, Mradi wa Maji na Ujenzi wa ghorofa 6 Hospitali ya Rangi tatu.
Miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 yote imepitishwa hakuna hata mradi mmoja uliokataliwa
Ifahamike kuwa Mwenge wa Uhuru 2024 unaongozwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg Godfrey Eliakimu Mnzava kwa Mkoa wa Dar es Salaam leo ni siku ya pili katika Wilaya ya Temeke, Mei 10 Mwenge wa Uhuru unaendelea Wilaya ya Kigamboni.