Juma lililopita niliandika juu ya pengo kubwa lililopo kati ya matajiri na maskini. Leo nagusia maskini wa dunia hii, wakulima, na jinsi gani wao wanaandamwa na mikakati kabambe ya kuwaongezea umaskini.

Taarifa ya hivi karibuni iliyochapishwa na Taasisi ya Oakland inaanika mbinu zinazoungwa mkono na Benki ya Dunia na wafadhili wa Nchimbi zinazoendelea za kuhimiza wakulima katika nchi maskini kuachana na matumizi ya mbegu asilia, na badala yake kuanza kutumia mbegu zinazotengenezwa na mashirika makubwa ya uzalishaji mbegu ulimwenguni.

Kampuni tano za kimataifa zilizopo kwenye nchi za Magharibi zinadhibiti zaidi ya asilimia 66 ya soko la mbegu rasmi ulimwenguni. Na katika miaka ya hivi karibuni kampuni hizi zimeongeza juhudi za kujipenyeza na kudhibiti soko la mbegu barani Afrika.

Athari zinazoelekea kuwakumba wakulima ni Marisol ya jitihada za kimkakati na sera ambazo zinaona kila tatizo linalokumba nchi maskini kuweza kupata suluhisho kwa kutumia wadau wa sekta binafsi.

Benki ya Dunia iliibua vigezo ilivyoviita Doing Business Index (DBI) kutathmini na kulinganisha urahisi wa kufanya biashara katika nchi mbalimbali ulimwenguni. Kwenye takwimu za hivi karibuni zilizotolewa Juni 2016, Tanzania inashikilia nafasi ya 132 kati ya nafasi 190 kwenye vigezo hivyo. Nafasi ya kwanza inashikwa na New Zealand, na ya mwisho inashikiliwa na Somalia. Tafsiri rahisi ya nafasi hii ni urahisi, au kukosekana kwa ukiritimba, kwa wafanyabiashara wanaokusudia  kuanzisha na kuendesha shughuli za biashara.

Kwa nchi maskini, kutimiza yale ambayo Benki ya Dunia inaona yanafaa ni sawa na kujihakikishia urahisi wa kuendelea kupata mikopo na misaada mbali mbali siyo tu kutoka Benki ya Dunia, bali pia kutoka kwa nchi na mashirika yanayofadhili mpango ya maendeleo katika nchi zinazoendelea.

Baadhi ya wachambuzi wameokosoa tathmini hii ya Benki ya Dunia na kuhimiza kwako ni kweli kuwa urahisi tu wa kuanzisha na kuendesha biashara unaweza kuleta matokeo chanya ya maendeleo. Aidha, baadhi ya wakasooaji wabainisha kuwa Benki ya Dunia inaipa nchi matokeo mazuri kadiri nchi inavyopunguza udhibiti kwenye sekta ya biashara.

Pamoja na mashaka juu ya faida za DBI, ni muundo huu ambao Benk ya Dunia inakusudia kuuleta kwenye matumizi ya mbegu katika sekta za kilimo za nchi zinazoendelea. Benki inadai kuwa upo ushahidi kuwa DBI inaweza manufa kwenye maendeleo ya kilimo ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha madai hayo.

Na ukiangalia mfumo wenyewe unaotumika, ni rahisi kuona ni kwa kiasi gani Benki ya Dunia inakuwa kinara wa kusimamia maslahi ya hizi kampuni chache ambazo zinatawala biashara ya kuuza na kusambaza mbegu.

Kwanza kabisa, kauli mbiu ya Benki ni kuwa mbegu zinazozalishwa na sekta binafsi ni teknolojia yaa msingi ya kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo. Zipo sifa chanya za mbegu zinazozalishwa na sekta binafsi, lakini zipo pia sifa chanya za mbegu asilia ambazo zimetumiwa na wakulima tangu enzi za mababu. Kwa kuweka msimamo huu, Benki inatoa nguvu kwa sekta binafsi kama ndiyo wadau pekee na muhimu katika sekta ya kilimo. Kwa msingi huu, wakulima, ambao ndiyo waathirika wakuu katika maamuzi haya, wanakuwa wapokeaji tu wa maamuzi yanayofanyika Washington DC.

Kwa kawida, serikali zingepaza sauti kutetea maslahi ya wakulima pale inapobidi, lakini hilo siyo rahisi kutokea. Katika ushauri wake, Benki ya Dunia inaziambia (neno linalotumika ni “kushauri”) serikali zianzishe kamati za kusimamia majukumu yafuatayo: kupitisha mbegu zinazozalishwa viwandani kwa lengo la kuziuza, kuandaa orodha ya mbegu zilizosajiliwa, na shughuli nyingine. Benki ndiyo inapanga vigezo vonavyopaswa kutimizwa na serikali, ikiwa ni pamoja na kushinikiza nchi zisitoze pesa nyingi kwenye usajili wa mbegu.

Aidha, Benki inashinikiza kuwa wajumbe wa kamati kutoka sekta binafsi easier pungufu ya asilimia 50 ya wajumbe wote. Hapa tunazungumzia sekta binafsi ambayo bila shaka itakuwa na uwakilishi wa yale makampuni makubwa kabisa ya kimataifa ambayo yanahodhi biashara ya mbegu ulimwenguni. Katika mfumo huu iwapo kamati inakuwa na wajumbe toka sekta ya umma pekee, wizara za kilimo au taasisi za utafiti, Benki ya Dunia inatoa alama ya sifuri kwa kamati hiyo. Ikiwa wajumbe wote watano wanatoka kwenye sekta binafsi nchi inapata alama zote.

Katika kuandaa muundo huu unaokusudia kuinua kilimo, Benki ilishirikisha wataalam kutoka kampuni kubwa duniani ziazozalisha bidhaa za sekta ya kilimo, ikiwa ni pamoja na Monsanto, Bayer, Syngenta, Pioneer, Yara, na KWS. Ingekuwa ni suala linaloruhusu kucheka, kitendo hiki kingetusababisha tucheke sana kwa sababu siyo tofauti na kwenda kwenye Hifadhi ya Serengeti na kuunda kamati ya wanyama wanaokula nyama na kuwaomba watoe ushauri wa kulinda maslahi ya wanyama wanaokula majani.

Ndani ya mfumo huu hakuna sehemu yoyote ambapo mkulima anawakilishwa. Na huu uwakilishi ni muhimu sana kwa sababu malengo ya mfumo huu ni kuongeza matumizi ya mbegu zinazozalishwa kiwandani pamoja na kupunguza mbegu asilia ambazo wamekuwa wanatumia wakulima. 

Baki kuwa waalishaji wa mbegu wanawakilishwa kwenye kamati, sheria pia zinatumika kulinda maslahi yao. Wazalishaji hawa wanatumia sheria za hatimiliki kupanga matumizi ya mbegu wanazozalisha, na matumizi haya huwa yanazuwia kutumia au kugawa mbegu hizo bila idhini ya mzalishaji. Ambapo ilikuwa kawaida kwa mkulima mmoja kwenda kwa jirani na kuazima mbegu kutoka kwa jirani yake, udhibiti unaowekwa na wazalishaji hawa utazuwia desturi hiyo. Kusudio la zuwio hilo ni kulazimisha wakulima kununua mbegu kila msimu ili kuongeza mauzo ya mbegu zilizosajiliwa.

Zipo nchi ambapo mkulima anayekiuka sheria zilizopo anaweza kutozwa faini au kutumikia kifungo. Kuna nchi kadhaa za Afrika ambapo ni marufuku kutumia mbegu ambazo hazijasajiliwa.

Rwanda na Vietnam wametumia mfumo wa EBA kutunga sheria mpya za mbegu. Na katika hatua zote za kusimamia mabadiliko kwenye sekta ya kilimo serikali zinalazimika kuzingatia mikataba ya kimataifa ambayo inalinda maslahi ya yale mashirika makubwa ya kimataifa yaliyosajili hatimiliki za mbegu.

Ni mzunguko ambao mkulima wa kawaida hana ubavu kukabiliana nao. Benki ya Dunia na wale wanaoitwa wadau wa maendeleo wanaweka taratibu ambazo zinaelezwa kuwa na madhumuni ya kuleta maendeleo ya kilimo, lakini ni taratibu ambazo, zaidi, zinalinda maslahi ya kampuni kubwa za kimataifa zilizopo kwenye biashara ya kilimo. Kwa kutumia nguvu yake Benki inashinikiiza serikali kuleta mabadiliko katika biashara ya mbegu, na ikibidi kutumia sheria kufanya hivyo, matokeo yake yakiwa si tu kuimarisha udbhibiti wa soko la mbegu kwa niaba ya hizo kampuni kubwa ila wakati huo huo kubomoa  kabisa maslahi ya wakulima.

Kama wapo maskini ambao wanaelekea kudidimizwa kabisa kwenye umaskini wao, basi wakulima wazi kuwa kwa mikakati hii inayoongozwa na Benki ya Dunia wakulima wamo miongoni mwao.