Leo Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua Skuli ya Maandalizi ya Tasani ikiwa ni muendelezo wa mchango wa Benki ya NMB katika kuchangia ukuaji wa elimu nchini.
Kwa kutambua mchango wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kuinua sekta ya elimu nchini, shule hiyo imepewa jina la Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika ufunguzi wa shule hii, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna alimueleza Mheshimiwa Rais kuwa:
Benki ya NMB imegharamia ujenzi wa skuli hii na uwekaji wa samani (ikiwemo viti, meza na madawati) kwa asilimia 💯 kwa gharama ya Shilingi Milioni 800.
Skuli ina madarasa matano na itaweza kupokea wanafunzi 200 kwa wakati mmoja. Pia imejumuisha ofisi za waalimu, sehemu ya michezo ya watoto na miundombinu mingine.
Tukiwa wadau wa karibu wa maendeleo nchini, tunaamini skuli hii itahaudumia vizazi ambavyo kwa baadae vitakuja kuleta mchango mkubwa katika maendeleo ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.