Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA
Shirikisho la soka Tanzania ‘TFF’ hatimaye limeweka bayana tarehe maalum za michezo minne ya hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu huu 2022/2023.
Taarifa hiyo muhimu imetolewa kupitia vyanzo vya habari vya shirikisho la soka Tanzania ‘TFF’ mapema Jumatatu ya Machi 20.
TFF imetangaza tarehe za michezo hiyo baada ya kupangwa kwa droo ya robo fainali mwishoni mwa juma lililopita kwa kushirikiana na wadhamini wakuu Azam Media.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mabingwa watetezi Yanga SC watacheza dhidi ya Geita Gold,April nane mwaka huu jijini Da es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kurejea kutoka DR Congo ikitoka kukabiliana na Tp Mazembe kwa mchezo wao wa mwisho wa kombe la shirikisho Barani Afrika.
Simba Sc nao watakabiliana na Ihefu FC April 07, jijini Dar es Salaam ikitokea nchini Morocco itakapokwenda kumenyana na Raja Casabalanca kukamilisha mchezo wao wa mwisho wa kombe la mabingwa barani Afrika.
Azam FC itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar April 03 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam, huku mchezo kati ya Singida Big Stars dhidi Mbeya City ukipangwa kupigwa April 02 mjini Singida kwenye Uwanja wa Liti.