Mfalme wa muziki wa aina ya Pop, Marehemu Michael Jackson, ametajwa kuwa kati watu maarufu duniani waliofariki dunia ambao kazi zao zimeingiza kiasi kikubwa cha fedha katika kipindi cha mwaka mmoja, kuanzia Oktoba 2012 hadi Oktoba 2013.

Kwa mujibu wa Jarida la Forbes la nchini Marekani, Bidhaa za Michael Jackson zimeonekana kununuliwa zaidi na kumfanya kuchukua nafasi ya kwanza kwa kuwazidi wasanii na watu wengine maarufu ambao walishafariki dunia lakini bidhaa zao bado zinaingiza fedha, hatua ya kuwazidi wale walio hai.


Kwa mujibu wa jarida hilo, Michael Jackson aliyefariki mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 50, bidhaa zake zimeingiza kiasi cha dola milioni 160 za Marekani. Bidhaa hizo ni pamoja na albam zake zenye nyimbo mbalimbali ambazo alitengenezwa wakati wa uhai wake.


Takwimu za Forbes pia zinaonesha kuwa, kiasi  hicho cha fedha mbacho ni kikubwa kimezidi  kile ambacho wameingiza wasanii maarufu ambao bado wako hai.


Katika jarida hilo unaonesha kuwa mwanamuziki maarufu duniani, Madonna ndiye mtu maarufu aliyetajwa kuingiza fedha nyingi zaidi kwenye  orodha wa watu maarufu akiwa ameingiza kiasi kiasi cha Dola milioni 125 za Marekani.