Na Jumanne Magazi,JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema shirika limepata mafanikio makubwa kiutendaji ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais DKt Samia Suluhu Hassan tokea aingie madarakani.
Akizungumza na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari katika ofisi za stesheni reli Dar es Salaam.
Kadogosa amesema katika kuelezea mafanikio yaliyofikiwa wameyagawa kwa sehemu sita ikiwa ni pamoja na vipaumbele vya shirika ndani ya miaka mitatu ya Rais Dkt Samia.
Aidha Kadogosa amesema kusudio kubwa ni kuelezea kilichofanyika ndani ya miaka mitatu ya Mheshimiwa Rais ikiwemo maendeleo ya ujenzi wa reli ya ya mwendokasi SGR, ikiwemo pia, maswala ya usanifu pamoja na ununuzi wa vitendea kazi vya mradi huo kama mabehewa na vichwa vya treni.
Aidha Kagodosa amesema “katika kujitathmini wao kama shirika walijipima na kujiringanisha na nchi za Afrika ambazo nazo zina miradi ya aina kama huu wa SGR lakini wamejiridhisha kuwa mradi huu utakuwa wakwanza barani Afrika”
Katika hatua nyingine mtendaji huyo,ameelezea jinsi gani ulivyomkubwa ukilinganisha na nchi nyingine zenye reli ya aina hiyo.
Reli ya SGR inakadiliwa kuwa na urefu wa kilometa 2000, ukiwa ni wa kwanza kwa ukubwa barani Afrika ikifanyiwa na nchi ya Morocco yenye reli ya kilomita 600.
Aidha Bw Kadogosa ameyataja mataifa mengine ya Afrika yenye reli ya mwendokasi kuwa ni pamoja na Kenya, Ethiopia ,Afrika ya Kusini.
Awali mkurugenzi huyo amezungumzia dira ya shirika hilo ikiwa ni kuifanya Tanzania kuwa lango kibiashara na kwa mataifa yanayoizinguka sambamba na kuongeza pato la Taifa kukuza uchumi wa Taifa kupitia miradi kikubwa ya reli ikiwemo hii ya SGR.
Bw Kadogosa ameendelea kufafanua kuwa hadi hivi sasa mtandao wa reli nchini umekuwa ukitoa huduma ya usafirishaji abilia kwa mikoa zaidi ya mikoa 16, Tanzania Bara .
Amesema hadi kufikia Februari mwaka huu shirika hilo lina mabehewa 100 kati ya hayo mabehewa 62 ni ya reli ya SGR.
Huku pia shirika likiwa linaendelea na ukarabati wa mabehewa mengine 200 ya reli ya zamani ambapo kwa sasa wanayakarabati kupitia utaratibu maalum na yale yaliyoshindikana wanayageuza kuwa chuma chakavu.
Bw Kadogosa amesema jumla ya gharama ya mradi huo ni zaidi ya kiasi cha shilingi za kitanzania Trilioni 23 ambazo zitakamilisha utekelezaji wa mradi huo huku Serikali ya Tanzania imeshamlipa mkandarasi kiasi cha shiringi Trioni 10 hadi sasa na kazi inaendelea na hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu wanatazamia reli hiyo itaanza kuhudumia Watanzania.