Matokeo rasmi yanaonesha Yamandu Orsi, ameshinda asilimia 49.81 ya kura iklinganishwa na Alvaro Delgado ambaye amejikingia asilimia 45.90 ya kura.

Rais mhafidhina wa Uruguay Luis Lacalle Pou amempigiaa simu na kumpongeza mgombea wa upinzani Yamandu Orsi kama rais mteule wa nchi hiyo ya Amerika Kusini na kumsaidia kuanza mchakato wa kukabidhi madaraka.

Lacalle Pou ameandika katika ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa X baada ya kura za maoni baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa kuonyesha kwamba Orsi angemshinda mgombea wa muungano unaotawala Alvaro Delgado, lakini kabla matokeo rasmi kutangazwa.

Delgado amekubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika jana Jumapili.