Na Tatu Mohamed, JamhuriMedia, Dodoma

TUME ya Nguvu za Atomu Tanzania, imetoa wito kwa Wakulima na wananchi kutembelea katika maonesho ya Nanenane ili kuweza kupata elimu kuhusu matumizi ya mionzi.

Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa Mionzi kutoka Tume ya nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Alphonce Mgina banda lao lililopo kwenye maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) kitaifa yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

“TAEC ni wadau wa wakubwa kwenye masuala ya Kilimo ambapo mionzi kwenye kilimo inatumika kuhifadhi chakula ili kiweze kukaa kwa muda mrefu. Lakini pia kupitia mionzi tumeweza kuua baadhi ya wadudu ambao ni wasumbufu.

“Kwahiyo kwenye maonesho haya TAEC imekuja kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuweza kupambana na mionzi kwa kuwa inafaida katika maisha ya binadamu na pia ikitumiwa visivyo huwa inaleta madhara. Na TAEC inajipambanua kwa ajili ya kuwasaidia wananchi ili waweze kupata huduma za mionzi hii kama wanaenda hospitali waweze kupata huduma za mionzi inayofaa,” amesema.

Ameongeza kuwa tume hiyo inaangalia mionzi kupitia vyakula ubora na uchafuzi hivyo TEAC imeweka vituo katika viwanja vya ndege bandari na mipaka kwa ajili ya kukagua vyakula vinavyoingia kama vimechafuliwa na mionzi.

Mgina ameeleza kuwa TEAC inaangalia vyakula vinavyosafirishwa kutoka nchini kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kulinda soko la Tanzania.

“TEAC imeweka watumishi wengi kwa lengo la kupambana na hili endapo kuna tatizo la mionzi tume inakuwa ya kwanza kupambana na tatizo hili,” amesema.

Please follow and like us:
Pin Share