Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam
Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SAC sekta ya afya wamekubaliana wanakuza mashirikiano ya pamoja kupitia bohari zao za dawa kutumia mfumo wa SADC Med Database (SMD) kufanya manunuzi ya bidhaa za Afya na vifaa tiba ili kurahisisha utoaji huduma na kupunguza gharama .
Ameyasema hayo leo May 14,2024 Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Afya John Jingu wa Uzinduzi wa mfumo wa taarifa (Med database) wa dawa na vifaa tiba zinazopatikana katika nchi za SADC hivyo mfumo huo utasaidia kufahamu bidhaa za afya zinapopatikana na gharama zake na muda wake wa matumizi.
“Mfumo huu wa taarifa (Med database) jumuiya yetu ya SADC utakuwa nyenzo muhimu katika sekta ya afya kwa bohari zetu za dawa tukiweza kuagiza dawa kwa pamoja nje ya nchi kwakuwa tutaagiza kwa wingi gharama itakuwa nafuu ” amesema Jingu.
Jingu amesema hadi kufikia hatua hiyo muhimu ni moja katima maongezi waliyokubalina viongozi wao katika majukaa mbalimbali na kupata baraka kuwa wanapoenda kufanya manunuzi ya bidhaa za dawa na vifaa tiba kwa pamoja itachoche kuvutia wawekezaji wa viwanda za bidhaa hizo muhimu.
Naye Afisa Mwandamizi Mfumo huo Calicious Tutalife amesema Tanzania kama kinara mwanachama wa kwakuwa mfumo huo umekuja kuzinduliwa nchini hapa hivyo ana imani kuwa watahamasishana ili mfumo usiishie kuongea bila utekezaji lazima wafikie hatua ya maamuzi hivyo mipango thabiti itawekwa na taarifa zote zitapatikana kupitia app mtandaoni kupitia simu ya mkononi.
Kwa Upande wake Mkurugenzi bohari ya dawa Tanzania Mavere Tukai amebainisha kuwa kanzi data hiyo hiyo ni nzuri ila bado inaendelea kufanyiwa kazi hatua kwa hatua ili ifikie kiwango cha kutoa huduma vizuri kutokana
“Hata mfumo wake wa utekelezaji ambao ulikuwa unaenda haukuweka mazingatio makubwa kwenye maeneo muhimu kama Sheri za manunuzi, Sheria za fedha pamoja na masuala ya udhibiti ubora, usajili wa bidhaa katika nchi husika na namna ya mfumo kufanyia kazi malipo kati ya mnunuzi na muuzaji” Amesema Mavere
Hata hivyo amesema wamefanya mapitio pamoja na wenzao wa Sekretarieti ya SADC ambapo wameangalia vitu vitano ikiwemo kubadilisha .taarifa za namna ambavyo wanatekeleza manunuzi ya pamoja, .