Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Tanga
SERIKALI ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imepata ufadhili wa Shilingi Bilioni 17 kutoka Mfuko wa Dunia wa Ufadhiliwa Huduma za Afya kwa ajili ya kuboresha huduma za wajawazito na watoto wachanga nchini ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo mkoani Tanga katika kikao kazi na wadau wa Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Ufadhili wa huduma za Afya ambapo Fedha hizo zitatumika kununua vifaa vya teknolojia, kuwajengea uwezo watoa huduma za afya madaktari, wauguzi, wakunga na watalaamu mbalimbali wanao hudumia wakina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga.
Katika vifaa hivyo mama mjamzito atavalishwa na vitaweza kusoma mapigo ya moyo ya mama mjamzito na mtoto aliyeko tumboni itasaidia kujua maendelkeo ya mtoto na mama mjamzito”, amesema Waziri Ummy
Akizungumza Mhe Ummy amesema awali mradi huo umetekelezwa katika mikoa mitano hapa nchini mbayo ni Manyara, Mwanza, Tabora ,Geita na Shinyanga katika hospoitali 150.
“Katika awamu ya kwanza mradio huu umeonyesha matokeo chanya kwa kupunguza vifoo vya mama na mtoto mchanga ambapo asilimia 25 vifo vitokanavyo na uzazi na asilimioa 50 watoto wachanga”, ameeleza Mhe Ummy
Vile vile amesema kuwa Utekelezaji wa mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na hospitari ya Lutheran ya Hydom iliyopo mkoni Manyara
Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassani ni kuokoa maisha ya watoto wachanga pamoja na mama wajawazito
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Mama na Mtoto Dkt Ahmad Makuwani amesema lengo la utekelezaji wa mradi huo ni kuhakikisha wakinamama wajawazito na watoto wachanga wanakuwa na maisha bora hapa nchini.
“Vifo vya mama mjamzito na watoto wachanga kwa Tanzania bado nijanga kubwa hivyo bado tunakazi kubwa ya kuhakikisha tunazidi kupunguza vifo hivi nchini”, ameeleza Dkt Makuwani
Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka Hospiy ya Hyidom iiliyoko mkoani Manyara Dkt. Paschal Mdoeamemshuku Waziri Ummy kwa ushirikiano aloutoa kwa hospital hiyo kutekeleza mradi huo katika mikoa mitano na kuleta matokeo chanya.