Siku ya juzi jumapili April 29, 2018 msanii Alikiba katika sherehe ya harusi yake iliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, alizindua kinywaji chake kipya kinachojulikana kama Alikiba Mofaya.
Kinywaji hicho ambacho hakina kilevi na chenye kuongeza nguvu (energy drink) kimewashangaza wengi kutokana na kuzinduliwa hafla tofauti na weni walivyotaraajia kuwepo kwa matangazo mbalimbali kabla ya uzinduzi wake.
Kutokana na uzinduzi huo, kumeibuka tetesi mbalimbali kuwa kinywaji hicho siyo mali ya Alikiba, ila yeye ni balozi tu, huku wengine wakidai kuwa Alikiba ndiye mmiliki wa kinywaji hicho.
Lakini kulingana na habari zilizopo, ni kwamba kinywaji hichi cha Mofaya kilizinduliwa nchini Afrika Kusini na DJ anayejulikana kwa jina Sabu.
Mtandao mmoja nchini Afrika Kusini uliandika
“South Africa dj and recording artist and television presenter dj sabu has created a new drinking energy known as MoFaya. Writing about new drinking on Facebook, the entertainer says# Mofaya to burn and melt all the nonsense in the fridge .skthathele .Finally a local brad is here. MoFaya has been 3 years in making , make sure you comply with the health standard and regulations .
The new drinking energy has been founded by eight South Africans,with a collective of 97 years of experience and every can sold will go towards educating a child in the region. Mofaya will take at least 100 students to university starting from 2016 and create at least 100 entrepreneur per years.”
Kufuatia ujumbe huo, watu wengi wamedhani kuwa Alikiba ni balozi tu wa kinywaji hizcho hapa nchini. Lakini katika ukurasa wa instagram wa mtengenezaji wa kinywaji hicho, Dj Sabu ameandika kuwa anafurahishwa kufanya kazi pamoja na Alikiba katika kutengeneza kinywaji hicho, na lengo lao ni kuhakikisha kuwa kinafiika katika maeneo yote ya Afrika.