Maafisa wa uokoaji nchini Taiwan wanatafuta meli ya mizigo iliyokuwa na wafanyakazi tisa ambayo imezama kwenye pwani yake ya kusini.

Meli hiyo yenye bendera ya Tanzania ilikuwa imetoka katika bandari ya kusini ya mji wa Kaohsiung wakati Taiwan ilipokumbwa na kimbunga Gaemi.

Dhoruba hiyo pia imesababisha mvua isiyoisha nchini Ufilipino, ambapo meli ya mafuta iliyokuwa imebeba takriban lita milioni 1.5 za mafuta ya viwandani imepinduka.

Wafanyakazi kumi na sita wa MT Terra Nova yenye bendera ya Ufilipino wameokolewa huku mmoja akiwa bado hajapatikana, Katibu wa Uchukuzi Jaime Bautista alisema.

Kimbunga Gaemi, ambacho kilitua pwani ya mashariki ya Taiwan siku ya Jumatano, kimewaua watu watatu na kuwajeruhi mamia zaidi katika kisiwa hicho, maafisa wamesema.

Kabla ya kupiga Taiwan, kimbunga Gaemi kilisababisha mvua kubwa nchini Ufilipino, ambapo watu wanane wamekufa.

Kinatarajiwa kusababisha kutua katika maeneo ya bara ya China baada ya kupita Taiwan.

Walinzi wa Pwani wa Taiwan wanasema meli hiyo ya mizigo, Fu Shun, iliyopinduka pwani yake, ilikuwa na raia tisa wa Myanmar.

Please follow and like us:
Pin Share