Timu za Simba na Azam leo zitakumbushia fainali ya Kombe la Mapinduzi ya mwaka 2017, wakati itakapo kutana katika hatua ya makundi
Azam FC na Simba zote za Dar es Salaam kesho zinatarajia kuchuana katika mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kwenye Uwanja wa Amaan hapa Zanzibar.
Mchezo huo ambao umepangwa kuanza majira ya 2: 15, unakumbushia fainali ya mwaka jana ya michuano hiyo ambapo Azam FC, iliibuka na ushindi wa bao 1-0, na kutwaa taji hilo kwa mara ya pili tangu kuanza kushiriki michuano hiyo ya Mapinduzi.
Timu hizo zinakuta zikiwa katika hali tofauti Azam ambao huo ni mchezo wa mwisho wa kukamilisha ratiba wameshafuzu hatua ya nusu fainali wakati Simba wanalazimika kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua hiyo ukizingatia pia inawaniwa na URA ya Uganda.
Pamoja na Azam tayari imefuzu kucheza nusu fainali lakini naamini haitokubali kupoteza mchezo huo kirahisi kwa kuiachia Simba, kocha Aristica Cioaba, anatarajiwa kupanga kikosi chake cha kwanza ili kuhakikisha wanapata ushindi.
Huo ni mtihani mtihani mgumu kwa kikosi cha Simba, ambacho kwa sasa kinanolewa na kocha Masoud Djuma, ambaye tangu amekabidhiwa majukumu
ya kuwa kaimu kocha mkuu amebadilisha mfumo wa uchezaji wa timu hiyo kwa kutumia 3-5-2 ambao umeweza kumsaidia kupata ushindi mnono wa
mabao 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Pemba jana.
Katika mchezo wa ligi timu hizo zipokutana uwanja wa Azam Complex Dar es Salaam, timu hizo hazikufungana na kuacha deni kubwa kwa makocha
wote wawili ambao hajapata matokeo dhidi ya mwenzake.
Azam ambao ndiyo wenyeji wa mchezo huo watakuwa wenyeji katika mchezo huo watakuwa na kikosi chao kamili na wanatarajia kufanya mashambulizi
mengi kupitia pembeni huku wakimtegemea zaidi mshambuliaji wake Bernald Arthur katika umaliziaji.
Winga Joseph Mahundi na nahodha Himid Mao, watakuwa na kazi moja ya kumtia majaribuni kipa Emmanuel Mseja ambaye kwasas ndiyo amepewa
jukumu la kuidakia Simba kwenye michuano hii baada ya Aishi Manula kuumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ndanda FC.
Simba kama walivyoingia kwenye mchezo dhidi ya Jamhuri juzi ndiyo inaonyesha itakuwa mara mbili yake kwasababu wanajua umuhimu wa
ushindi katika mchezo huo ambao ndiyo utawapa tiketi ya kuendelea kubaki kwenye michuano hiyo.
Kocha Masoud Djuma, niwazi atalazimika kuongeza idadi ya viuongo kwenye kikosi chake ili kuwadhibiti Azam FC, kwenye eneo la kati kati
ya uwanja na kumpa kazi nyepesi mshambuliaji wake John Bocco kuidhuru timu yake ya zamani.
Bila shaka Djuma atamwanzisha Bocco, kwasababu ndiyo mshambuliaji aliyeonyesha kuwa na imani naye sambamba na chipukizi Moses Kitandu
ambaye naye ameonekana kuwa na mwendelezo mzuri katika umaliziaji.
Vita kali katika mchezo huo litakuwa kwenye eneo la kiungo ambapo Stephen Kingue,Mao, Joseph Mahundi na Enock Agyei watakuwa na kazi ya
kuwadhibiti viungo wa Simba Mwinyi Kazimoto, Mzamiru Yasini, Shiza Kichuya na James Kotei wasiweze kupeleka madhara langoni mwao.
Lakini pamoja na yote walinzi wa Azam wanapaswa kumchunga beki Asante Kwasi kutokana na ujanja wake wa kupanda kusaidia mashambulizina na
kufunga kama ilivyotokea kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Jamhuri.
Kulingana na ubora wa timu zote mbili mchezo huo unatarajiwa kuwa wakuvutia na hesabu zaidi na mashabiki wa soka wanausubiria kwa hamu
ili kujionea kile kinachokwenda kutokea kwenye uwanja wa Amaan.