Na Magrethy Katengu,Jaa8huriMedia Dar es Salaam
NAIBU Katibu Mkuu Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Wilbroad Mastai, amewashauri vijana kuwa waangalifu na mitandao ya kijamii kwa kuwa uharibifu mkubwa wa kidunia umeelekezwa huko ili washindwe kutimiza ndoto zao.
Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam Juni 13 ,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kundi hilo ni kubwa lina nguvu na lina ndoto nyingi za kutimiza hivyo ibilisi anashughika nalo kila siku ili aweze kuliangusha amewasihi Wazazi, walezi ni budi kutimiza wajibu wao wa malezi pasipo kubagua jinsia kwani sasa Mtoto wa kiume yupo hatarini zaidi asisahauliwe kiulinzi kama ilivyokuwa hapo awali.
“Dunia inawatafuta wao kwa kuwa ni kundi kubwa na lina ana nguvu na ndoto nyingi maana ukiangalia Taifa lolote mahali popote ukitaka kufanya chochote lazima watafute vijana hivyo muhimu nyumba za ibada kusaidia kundi hilo kwani sasa Ombwe lililoibuka ndoa za jinsia moja ikiwemo Ushoga na Usagaji wanatumia mitandao ya kijamii kuwashawishi wao” amesema Mchungaji Mastai.
Aidha ili kusadia hilo Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania limekuwa na likiwakusanya kila mwaka mara moja katika Tamasha la Twenzetu kwa Yesu kwa kuwapa mafundisho kuanzia asubuhi mpaka jioni ambapo mwaka huu Juni 15, 2024 litaanza.