Mchungaji wa Kiprotestanti Docho Eshete aliyekuwa akibatiza watu katika ziwa Ayaba kusini mwa Ethiopia ameuawa na mamba. Mashambulizi yaliyo karibu na mji wa Arba Minch yanahusishwa na kupunguza idadi ya samaki ambacho ni chakula cha Mamba na hivyo kuanza kuvamia watu na kuwaua.

Mchungaji, Docho, ndo kwanza alikuwa ameanza kumbatiza mfuasi wa kwanza kati ya themanini waliokwenda kufanyiwa huduma hiyo katika ziwa Ayaba, huko Ethiopia wakati mamba aliporuka nje kutoka majini na kumchukua mchungaji huyo.

Mchungaji alijitahidi kupambana na kujiokoa na mashambulizi ya mamba huyo ambaye alikuwa amemsababishia majeraha makubwa.

Wakazi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na wavuvi walijaribu kutumia nyavu ili kumuokoa na mamba huyo asimwingize kwenye kina kirefu ndani ya ziwa hilo lakini hata hivyo juhudi zao hazikuweza kuokoa maisha ya mchungaji huyo na walichoweza ni kuopoa mwili wake baada ya kuwa tayari amefariki.

Watu wanaoishi karibu na ziwa hilo katika mji wa Arba Minch wanasema uvuvi uliopindukia umesababisha kupungua kwa chakula cha mamba na matokeo yake mamba wamekuwa wakionekana wakiwinda kando kando ya Ziwa