Na Lookman Miraji,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo kutoka nchini Ufaransa ya Sergio Mat imekabidhi rasmi vifaa vya michezo kwa timu ya taifa ya mchezo wa raga nchini.

Hafla ya tukio hilo limefanyika Septemba18 katika eneo la wazi la mgahawa wa slow Leopard ulioko Masaki Dar es Salaam.

Tukio hilo limefanyika mara baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Chama cha Mchezo wa Raga nchini na kampuni hiyo ya utengenezaji vifaa vya michezo kutoka nchini Ufaransa.

Tukio hilo liliongozwa na ofisa kutoka Baraza la Michezo la taifa BMT Charles Maguzu.l ambapo ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa timu ya taifa ya raga ya wanawake na kuiomba kampuni kuendelea kusaidia michezo nchini.

Mbali na salamu hizo za shukrani afisa Maguzu amewapongeza viongozi wa chama cha mchezo wa raga nchini na kwani wameonyesha kwa vitendo dhana ya mashirikiano ya kimataifa katika kuendeleza michezo kwani jambo hilo lisingiwezekana bila wao kuwa na mahusiano mazuri na kampuni hiyo kutoka nchini Ufaransa.

Aidha Maguzu ameongeza kwa kutoa ahadi kwa niaba ya BMT kuwa watashirikiana na viongozi wa mchezo wa raga kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa na kutumika kwa kadri inavyotakiwa kwa kuandaa timu ya taifa ya wanawake na kuhakikisha kuwa wanashiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Pia kwa upande wa chama cha mchezo wa raga nchini kupitia Rais wake Jacob mbali na shukrani alizozitoa kwenda kwa Kampuni ya Sergio mat ameeleza kuwa wao kama viongozi wanalo jukumu kubwa kuhakikisha wanaunda timu imara ya taifa ya mchezo wa raga.

Akizungumza naye mkuu wa maendeleo ya wanawake katika mchezo huo wa raga nchini Fatma el kindiy amesema kuwa kupitia vifaa hivyo itafungua milango kwa wachezaji wa mchezo huo kuzidi kujitangaza katika soko la kimataifa kimichezo hususani kwa wanawake.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa leo hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya mchezo wa raga nchini kwa timu ya taifa ya wanawake wa mchezo huo kuwa na vazi maalum la michezo.