Na Lookman Miraji, JamhiriMedia, Dar es Salaam
Mchezo wa raga nchini umeibuka na taswira mpya ya kimataifa mara baada mchezo ya mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania na timu ya maveterani kutokea nchini Uingereza.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa umechezwa huku ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuimarisha uhusiano na urafiki baina ya mataifa hayo mawili katika michezo hususani kwa upande wa mchezo wa raga.
Akizungumza Rais wa chama cha mchezo wa raga nchini, Bwn: Joseph Jacob amesema kuwa kupitia mchezo huo wa kirafiki wameuchukulia kama sehemu ya motisha kwao kwa kuendelea kutengeneza kikosi cha ushindani kitakachoiwakilisha nchi.
“Tumefurahi kwa mchezo huu kwani umekuja wakati sahihi kwetu na hii tunachukulia kama motisha kwetu ya kuendelea kutengeneza kikosi kitakachotuwakilisha kama timu ya taifa kama Tanzania.”
Kwa upande mwingine pia mchezaji wa timu ya maveterani hao wa Tritons Tony Dunkerley nae ameonesha kufurahishwa na mchezo ulioonyeshwa na timu ya Tanzania huku akikiri kuwa walizidiwa ubora katika maeneo mengi.
“Kiukweli tumefurahia mchezo japo matokeo ni tofauti ila mchezo umetoa mshindi wa kweli. Tanzania walikuwa vizuri wameonyesha ujuzi na walikuwa na kasi pamoja ari ya ushindani kiukweli wamecheza vizuri na sisi tulizidiwa ” Alisema.
Mchezo huo ulimalizika kwa Tanzania kushinda kwa pointi 38 dhidi 20 za timu hiyo Tritons kutoka nchini Uingereza.