Na Isri Mohamed
Mchezaji wa klabu ya Kafr El Sheikh SC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri, Mohamed Shawky amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla uwanjani wakiwa kwenye mechi ya ligi dhidi ya Kazazeen iliyochezwa Novemba 14, 2024.
Madaktari wa klabu yake walijaribu kumtibia Shawky (26) uwanjani hapo lakini ikashindikana, ndipo walipokimbiza katika Hospitali ya Zarqa kwa matibabu Zaidi.
Baada ya kufikishwa Hospitali, Shawky alilazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi na ilibainika alipata mshtuko wa moyo.
Akiendelea kupatiwa matibabu, moyo wake ulisimama ghafla akiwa kwenye mashine ya kupumulia, ambapo Madaktari walifanya juhudi kubwa za kufufua mfumo wake wa moyo na mapafu bila mafanikio.
Shawky alifariki dunia saa 4:00 asubuhi Jumanne ya Novemba 19, 2024.