Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Mbunge viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jackline Ngonyani Msongozi ameiomba serikali kupitia wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuona umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa Barabara ya Mtwara corridor (Songea by pass) ambayo itasaidia kuondoa msongamano wa maroli katikati ya mji ,yanayosafirisha makaa ya mawe kutoka Mbinga kwenda mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuacha kuchafua mazangira kwa kumwaga makaa ya mawe ovyo barabarani.

Alisema kupitia siku hii ya kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, wanaomba kuharakisha kwa ujenzi wa barabara hiyo kwani hali ni mbaya kutokana na ongezeko la maroli hayo kupita katikati ya mji kunasababisha adha kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo jambo ambalo linaweza kusababisha ajali , ambapo ameitaka mamlaka husika kuharakisha ujenzi wa barabara ya mchepuko ya Mtwara cordo ili kuondoa kero hiyo.

Wanawake wa Mkoa wa Ruvuma wakipita na maandamano mbele ya mgeni rasmi kwenye uwanja wa Maji Maji Songea.

“Tunaiomba serikali iharakishe mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara cordo ambao utasaidia kuondoa msongamano wa Maroli kwenye barabara kuu itokayo Mbinga-Songea -Njombe ili kuondoa usumbufu wa msongamano wa maroli ambayo yamekuwa mengi zaidi na kuhatarisha maisha ya watumiaji wakiwemo mama lishe,wafanya biashara na kuturahisishia shuguli zetu za kila siku kama zamani,”. alisema Msongozi.

“nichukuwe nafasi hii kuomba serikali ifanye wepesi wa kutengeneza barabara ya by pass ya Songea manispaa kumekuwa na changamoto kubwa sana ya ajari za barabarani hapa katikati ya mji,maroli yanapita hapa, msongamano ni mkubwa sana, sasa kupitia hadhara hii sisi wanawake ndio ambao tunaguswa moja kwa moja na changamoto na msongamano huu,mwanamke anatoka mshangano anatakiwa akimbizwe kwenda hospitali ya Wilaya kwa haraka kwenda kujifungua lakini anashindwa kwaajiri ya msongamano wa maroli” alisema.

Alisema maroli hayo yamekuwa yakipita kwa mwendo kasi hata kwenye maeneo yenye makazi ya watu bila kujali watumiaji wengine wa barabara na kusababisha ajali mbaya ambazo zingeweza kuzuilika kama kungekuwa na barabara ya mchepuko.

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jacklin Ngonyani Msongozi akihutubia siku ya kilele cha wanawake kimkoa imefanyika Manispaa ya Songea.

kwa upade wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile alisema kuwa serikali tayari imeshatenga fedha za barabara hiyo kutoka Kata ya Mletele kuzunguka Msamala kwenda Namanditi ili maroli yanayopita barabara kuu Songea-Njombe yaache kupita kwa sababu yanasababisha ajari.

” kutokana na ongezeko la Maroli ya makaa ya mawe tunataka barabara ya mchepuko ipite kuanzia Mletele ,kuzunguka Msamala hadi Namanditi kupitia barabara ya Tunduru Masasi, ambapo kikubwa ni kupunguza msongamano wa kupita kwenye makazi ya watu hasa maeneo ya mjini.” Alisema Kapenjama.

Aidha, ameongeza kuwa maradi huo unajengwa kupitia Benki ya Dunia ,ambapo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kipindi mradi utakapoanza kwani mradi huo ni wao pia wasafirishaji kushirikiana waache kuharibu miundombinu na kuchafua barabara kwa kumwaga ovyo makaa ya mawe barabarani.

Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Jacklin Ngonyani Msongozi