Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kuwa, wanawashikilia askari 6 ambao wametumia silaha za moto katika uchaguzi huu mdogo wa Kinondoni.
Aidha, Mambosasa amesema kwamba, CHADEMA waliwazuia Polisi kutekeleza wajibu wao ndio sababu nguvu ya ziada ilitumika kutawanya waandamanaji.
Amesema wanamtafuta Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe ili wamfikishe katika vyombo vya sheria.
Hadi sasa wafuasi wa CHADEMA 40 wamekamatwa na wanashikiliwa mpaka sasa kwa kuandamana katika uchaguzi wa marudio.