Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Wakati mbio za Uchaguzi katika ngazi ya mkoa kichama kwa Chama Cha ACT Wazalendo, zikiwa zimezinduliwa jana kwa mikoa miwili ya Tanga na Morogoro kufanya uchaguzi, sura mpya zimejitokeza ndani ya nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwaondoa wakongwe waliokuwa wakishikilia nafasi za uongozi kabla ya uchaguzi huo.
Katika Mkoa wa Tanga,Mwenyekiti mpya wa ACT Wazalendo aliyechaguliwa ni Hamis Issa Kunga aliyepata kura 98 dhidi ya Mshindani wake wa Karibu Abdulrahmani Bakari Lugone aliyepata kura 70.
Nafasi ya Katibu wa chama mkoa imechukukiwa na Musa Kasim Mbega, aliyepata kura 89,dhidi ya mshindani wake Hamad Ayoub Kidege aliyepata kura 74.
Kabla ya uchaguzi huo wa jana Lugone alikuwa ni Katibu wa Mkoa waTanga ACT Wazalendo,huku Kidege akiwa ni Mwenyekiti wa Clchama mkoa.
Nafasi ya matibu wa mipango na uchaguzi imeenda kwa Mustapha Ally,aliyepata kura 103 dhidi ya Kibibi Bakari Mwalimu aliyepata kura 65.
Nafasi ya jenezi mkoa imechukuliwa na Omari Rashid Omari aliyepata kura 106 dhidi ya Peter Julius Rujiama aliyepata kura 62.
Nafasi ya mweka hazina wa mkoa iligombewa na mgombea mmoja pekee Ramadhan Kilatu,aliyepata kura 162 baada ya wajumbe kumpigia kura
Nafasi ya wajumbe wawili wanawake, zilikwenda kwa Aziza Muhaka Chambega na Zaina Rashid Mahanyu ambao hawakuwa na wapinzani na kila mmoja alipata kura 168
Katika nafasi ya wajumbe wawili wanaume walijitokeza wagombea wanne,ambapo waliochaguliwa ni Abdarahman A.Hassa aliyepata kura 94 na Bryson Peter Mwanzazila aliyepata kura 99.
Wagombea wengine walijitokeza katika nafasi hiyo ni na kura zao hazikutosha ni Tajiri Mbwana Mwinchumu aliyepata kura 68 na Hussein Elisiagi aliyepata kura 78.