Uongozi wa Mbeya City umesema tayari umeshajiandaa vizuri kuelekea mchezo wa leo wa ligi dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga imewasili mjini humo jana ikiwa ina kibarua leo dhidi ya wenyeji wao Mbeya City, na ikiwa ni siku kadhaa wakiwa wametoka Ethiopia kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Mbeya City, Shaha Mjanja, amesema kuwa wapo tayari na wamejikamilisha vilivyo kuondoka na alama tatu kwenye mtanange huo.
Jeuri hiyo ya Mbeya City imekuja kwa kudai kuwa wamejipanga vema na Yanga hatoweza kupata matokeo kwa namna yoyote.
“Tumejipanga vizuri, Yanga hawezi kuondoka na alama tatu kwa kuwa vijana wetu wapo vizuri kushinda mechi ya leo” alisema Mjanja.
Mchezo utaanza majira ya saa 10 kamili jioni na utarushwa mbashara na kituo cha Azam TV.