Baraza la mawaziri la usalama la Israel limemuidhinisha hatua ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na waziri wake wa ulinzi ya kuamua ni lini na jinsi ya kulipiza kisasi cha shambulio baya la roketi dhidni ya Israel na Marekani inasema lilitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Kishia wa Lebanon Hezbollah.

Mawaziri walikutana katika kikao cha dharura kufuatia shambulio hilo lililifanyika kwenye Milima ya Golan inayokaliwa na Israel Jumamosi jioni, lililowauwa watoto na vijana 12 kutoka jamii ya Druze. Hezbollah imekana kuhusika.

Lilikuwa ni tukio baya zaidi la shambulio la kuvuka mpaka kuwahi kufanyika katikakipindi cha miezi kadhaa ya makabiliano ya silaha kati ya pande hizo mbili.

Shambulio hilo limeongeza hofu kwamba mapigano ambayo yamedhibitiwa hadi sasa yanaweza kuenea na kuwa vita kati ya pande mbili.

Serikali za Magharibi zinaitaka Israel ijizuie katika kujibu kwake shambulio hilo.

Ikulu ya White House imesema imekuwa katika “majadiliano endelevu na wenzao wa Israel na Lebanon tangu shambulio la kutisha” liliporokea kwenye uwanja wa michezo katika kitongoji cha Druze kilichopo katika mji wa Majdal Shams.

Please follow and like us:
Pin Share