Meza ya Majaji ambapo wamekaa Jaji Mkuu, Jaji Mkuu Kiongozi pamoja na majaji wengine.

Taswira ilivyoonekana katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya mawakili wapya walioapishwa leo wakiwa sehemu yao iliyoandaliwa.

Mmoja wa mawakili akitoa nasaha kwa mawakili hao.

ZAIDI ya mawakili 80 wamehitimu mafunzo na kuapishwa kuanza kazi ya kuhudumu kama watetezi wa kisheria katika mahakama mbalimbali hapa nchini huku Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof Ibrahim Juma akitia neno juu ya kuhakikisha wanatumia taaluma yao kusaidia jamii na kujiendeleza zaidi ili kufahamu sheria mpya zinazosimamia mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Prof Ibrahim ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha mawakili hao wapya wa mahakama kuu Jijini Dar es salaam, ambapo amewataka mawakili hao kujiepusha na vitendo vya rushwa na pia kufanya kazi zao kwa weledi ili kulinda heshima ya taaluma hiyo.

 

Baadhi ya mawakili wahitimu, Theresia Masha na Frank Kimaro wameelezea namna ambavyo watatumia taaluma yao katika kuwahudumia wananchi na hasa wenye matatizo ya kisheria na kwamba watahakikisha wanatenda haki katika majukumu yao ya kikazi.