Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia, Dar es Salaam
Sekta ya elimu inatakiwa kuja na mikakati mizuri ya Tehama ili kusaidia weledi wa ufundishaji kwa kuangalia mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kasi ili kurahisisha shughuli zake na kuwa na weledi.
Hayo yamebainishwa leo Juni 24,2024 Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Carolyne Nombo katika kikao kazi cha siku mbili na wadau mbimbali wa elimu kutoa maoni ya Mjadala wa Kitaifa juu ya rasimu ya mkakati wa kitaifa wa matumizi ya teknolojia za kidigital katika Elimu ambapo amesema Dunia inaenda kasi kila kitu kipo kidigitali hivyo kwakuwa sekta ya elimu ndiyo inayozalisha wabunifu na watafiti wengi tehama ni muhimu sana kwao.
“Sote tunafahamu kuwa Dunia ni ya kidigitali kutokana na sayansi na teknolojia hivyo ni budi kufanya maboresho katika sekta mbalimbali hasa sekta ya elimu kwa kuweka mifumo madhubuti ya utoaji elimu uwe wa kidigitali”Amesema
Hata hivyo amebainisha kuwa Serikali imekuwa mstari wa mbele kugawa vifaa vya teknolojia kila shule yaani Vishkwambi kwa waalimu ili waweze kufundisha wanafunzi kidigitali ,vilevile miaka miwili iliyopita waliweza kupokea maoni juu ya kuboresha elimu ya Tanzania na wadau walihamasisha utoaji ufundishaji uwe wa kidigitali.
Naye Mwanafunzi wa Kidato cha tatu Grace Kunambi ametoa maoni yake kwa kusema kuwa mkakati huo wa kitaifa kwao una umuhimu akitolea mfano somo la hesabu baadhi ya silabasi kuna kifaa cha kiteknolojia na wanaambiwa wakinunue ili kiwasaidie wanapofanya maswali hivyo ingependeza hata masomo yote wangefundishwa kwa kutumia teknolojia ili wawe wabunifu wasisubirie mpaka wafike vyuo.
Simoni Migile teknolojia ni muhimu sana kwa waalimu wanaowafundisha mashuleni inapunguza ghrama ya kununua chaki kuandika ubaoni hivyo Serikali iliangie suala hilo kwa jicho la umakini kwa kupeleka vifaa vingi vya teknolojia mashuleni ili wawe wanasoma online kwani sasa wakiangalia Dunia inaenda kasi kidigitali .