Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amesty International nchini Kenya limeripoti kutekwa kwa Mwanaharakati na Mtetezi wa Haki za Binadamu Mtanzania Maria Sarungi Tshehai leo katika eneo la Kilimani jijini Nairobi Nchini Kenya.

Taarifa ya Shirika hilo imesema watekaji hao wamefanya tukio hilo  saa 15.15 alasiri wakiwa ni wanaume watatu wenye silaha wakiwa na gari jeusi aina ya Toyota Noah ambapo shirika hilo limeomba watu mbalimbali kupaza sauti zao juu ta tukio hilo ili kumsaidia Maria kuwa salama.