Masoko ya hisa barani Asia yameshuka baada ya mauzo ya hisa nchini Marekani kupanda kutokana Rais Donald Trump kutotoa hakikisho kwamba ushuru wake unaweza kusababisha mdororo katika uchumi mkubwa zaidi duniani.
Kuporomoka kwa hisa hizo kumefuatia maoni ya Trump kwamba uchumi wa Marekani uko katika “kipindi cha mpito”, alipoulizwa kuhusu wasiwasi juu ya uwezekano wa kushuka kwa uchumi.
Maelezo ya picha,Soko la hisa la China liliporomoka kutokana na wasiwasi wa kauli ya Trump
Rais huyo hajazungumzia moja kwa moja kuhusu uchumi tangu atoe kauli hizo, lakini viongozi wake wakuu na washauri wametaka kutuliza hofu ya wawekezaji.
“Dhana ya awali ya Trump kuwa rais wa soko la hisa inatathminiwa upya,” alisema Charu Chanana, mtaalamu wa mikakati ya uwekezaji katika benki ya uwekezaji ya Saxo aliiambia BBC.
Katika mahojiano na Fox News yalichapishwa Jumapili baada ya kurekodiwa Alhamisi, Trump alionekana kukiri wasiwasi juu ya uchumi. “Sipendi kutabiri mambo kama hayo,” alisema. “Kuna kipindi cha mpito kwa sababu tunachofanya ni kikubwa sana. Tunarudisha utajiri wa Marekani. Hilo ni jambo kubwa.”aliongeza.
