Raia watatu wameuawa Jumapili katika shambulizi la makombora lililofanywa na kikosi cha RSF katika eneo la Omdurman karibu na Khartoum, siku mbili tu baada ya jeshi la Sudan kutwaa tena ikulu ya rais katika mji mkuu huo.

Raia watatu wameuawa Jumapili katika shambulizi la makombora lililofanywa na kikosi cha RSF katika eneo la Omdurman karibu na Khartoum, siku mbili tu baada yajeshi la Sudan kutwaa tena ikulu ya rais katika mji mkuu huo.

Mashuhuda walisema mashambulizi hayo ni miongoni mwa mabaya zaidi katika miezi ya karibuni, ambapo watoto wawili na mwanamke mmoja waliuawa huku wengine wanane wakijeruhiwa.

Tangu Aprili 2023, vita kati ya jeshi la serikali na RSF vimesababisha vifo vya makumi ya maelfu, huku watu milioni 12 wakilazimika kuhama makazi yao, na kuibua mzozo mkubwa wa njaa na ukimbizi duniani.

Licha ya jeshi kupata ushindi muhimu mjini Khartoum, wachambuzi wanaonya kuwa mapigano yanaweza kuendelea kwa muda mrefu kutokana na RSF kushikilia maeneo mengine nchini humo na kuendelea kushambulia raia, hasa katika jimbo la Darfur.