Israel imezidisha vita vyake dhidi ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon Septemba 23, huku vita hiyo ikiua takriban watu 490 na kujeruhi wengine zaidi ya 1,650 katika mashambulizi makubwa ya anga ambayo yamezua wasiwasi wa kutokea vita vikali.
Jeshi la Israel lilishambulia zaidi ya ngome 1,300 ambapo shirika la habari la serikali ya Lebanon likiripoti mapigano makali katika majimbo mengi eneo la kusini mwa nchi.
Katika ripoti iliyotoka kwa Maafisa wa wizara ya afya ya nchini Lebanon inaonyesha miongoni mwa waliouawa katika vita hiyo ni watoto 35 na wanawake 58.
Pia Jeshi la Israel limeonya wakazi wa bonde la Bekaa mashariki mwa Lebanon kukaa mbali na ghala za silala za Hezbollah.
Msemaji wa jeshi la Israel Amirali Daniel Hagari aliwambia waandishi wa habari kuwa wanaendelea na maandalizi ya Hezbollah uwanjani ili kuzuia mapema mashambulizi yao kwenye eneo la Israel.
Katika ujumbe uliorekodiwa kwa raia wa Lebanon, waziri mkuu wa Israel Banjamin Netanyahu amewataka kuzingatia wito wa Israel wa kuondoka, akisema lazima “wachukulie onyo hilo kuwa sio mzaha”