Marekani imekabidhi kambi yake ya mwisho ya kijeshi kwa mamlaka ya Niger.

Kambi hiyo ilikuwa mojawapo ya vituo viwili muhimu vya Marekani katika mapambano yake ya kukabiliana na ugaidi.

Wizara za Ulinzi za Marekani na Niger zilitangaza kwenye taarifa ya Pamoja hapo jana Jumatatu baada Marekani kukabidhi kambi ya kijeshi nambari 201 katika jiji la Agadez.

Mapema mwezi huu wanajeshi wa Marekani waliondoka kutoka kwenye kambi nyingine ya wanaanga nambari 101, kambi hiyo ndogo ilikuwa ni kituo cha ndege zisizo na rubani katika mji mkuu wa Niger, Niamey.

Wanajeshi wa Marekani wana hadi Septemba 15 kuondoka katika nchi hiyo ya Sahel baada ya kufikia makubaliano na serikali ya Niger.

Please follow and like us:
Pin Share