Maafisa wa Marekani na Urusi wamekamilisha mazungumzo ya siku moja jana Jumatatu, wakiangazia pendekezo la mapatano ya kusitisha vita baharini kati ya Kyiv na Moscow, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kidiplomasia zinazonuwiwa kuchangia mazungumzo mapana ya amani.
Lakini hata wakati mazungumzo hayo yakiendelea nchini Saudi Arabia, ambapo ujumbe wa Ukraine ulikuwepo, kombora la Urusi lilipiga shule na hospitali nchini Ukraine, na kujeruhi watu wasiopungua 88.
Mazungumzo hayo yalilenga makubaliano ya kusitisha mapigano katika Bahari Nyeusi, na baadhi ya taarifa zilisema kuwa yalikuwa yanapiga hatua na kulitarajiwa kutolewa tangazo chanya hivi karibuni.
Wiki iliyopita Urusi ilikataa mapendekezo ya Trump ya kusitisha kabisaa vita kwa siku 30, ikikubali tu mapatano ya kutoshambulia miundombinu ya nishati.
Mazungumzo hayo pia yamejadili masuala ya mipaka, na umiliki wa mitambo ya umeme, kulingana na Rais wa Marekani Donald Trump.
